Akiongea na East Africa Radio, Dkt. Mgasa amesema kuwa ongezeko hilo limetokana na kuwepo kwa elimu miongoni mwa jamii juu ya kuchangia damu kwa hiari na wananchi wengi kuonekana kuitikia wito wa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wengine.
Dkt. Mgasa ametoa takwimu za makusanyo ya damu ambapo amesema katika kipindi cha mwezi Januari jumla ya chupa za damu 2,534 zilichangwa ambapo mwezi Februari chupa 2,612 na kwa mwezi Machi chupa 3,368 zilichangwa na kupungua kwa uhaba wa damu katika hospitali za Kanda ya Mashariki na kuwataka wananchi waendelee kuchangia damu kwani mahitaji halisi ya damu kwa jiji la Dar es salaam ni chupa 4,000 kwa mwezi, wakati huko nyuma zilikuwa zinapatikana chupa 2,000 pekee kwa mwezi.






