Bradley Beal kuyakosa mashindano ya Olympic 

Ijumaa , 16th Jul , 2021

Nyota wa mpira wa kikapu wa timu ya taifa ya Marekani, Bradley Beal atakosekana kwenye mashindano ya Olympic yatakofanyijka Julai 23 mwaka huu kwenye mji wa Tokyo nchini Japan baada ya nyota huyo kuwa karibu na mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa huo.

Bradley Beal wa timu ya taifa ya Marekani na klabu ya Washington Wizard ambaye atakosekana kwenye mashindano ya Olympic mwaka huu nchini Japan.

Beal anakosekana kwani taratibu za NBA za kujikinga na Covid-19 linamtaka mtu aliyehusiana na mtu mwenye ugonjwa huyo kukaa karantini kwa siku zisizopungua kumi, siku ambazo michuano hiyo itakuwa imeanza tayari na Marekani kukipiga nja Ufaransa Julai 25, 2021.

Baada ya Beal kuthibitika kukosekana, kocha wa timu ya taifa ya Marekani, Cregg Popovich amesema ameumizwa sana na taarifa hizo kwani Bradley alionesha mchango mkubwa kwenye kikosi hicho kwenye michezo ya kirafiki dhidi ya Australia na Nigeria.

“Bradley, hakuna mashaka ni pengo kubwa. Alikuwa anacheza vizuri sana, anaelewa kila kitu na alifiti vizuri kwenye timu”. Popovich amesema.

Ikumbukwe kuwa Bradley Bill ni mchezaji wa pili kwa kufunga sana kwenye msimu mzima wa NBA akiwa na wastani wa kupata alama 31 kila mechi nyuma ya Stephen Curry wa Golden State Warriors ambaye pia amejumuishwa pia kwenye kikosi hicho.