Wakurugenzi wanne MSD wasimamishwa kwa ubadhirifu
Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto imeagizwa kusimamishwa kazi kwa wakurugenzi wanne wa Bohari Kuu ya Dawa nchini Tanzania MSD kufuatia ubadhirifu wa shilingi bilioni 1.5 kubainika.
