Monday , 15th Feb , 2016

Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto imeagizwa kusimamishwa kazi kwa wakurugenzi wanne wa Bohari Kuu ya Dawa nchini Tanzania MSD kufuatia ubadhirifu wa shilingi bilioni 1.5 kubainika.

Agizo hilo la kusimamishwa kazi kwa wakurugenzi hao limetolewa leo jijini Dar es salaam na waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu wakati akipokea na kusimamia kufungwa kwa vitanda vipya katika wodi ya wakina mama baada ya agizo la Rais alilolitoa Alhamisi wiki iliyopita.

Akiongelea idadi ya vitanda vilivyotolewa Ummy amesema kuwa jumla ya vitanda 120 vimetolewa kwa wagonjwa wa kulala na vitanda kumi vya kujifungulia pamoja na vitanda kumi vya watoto njiti na kuagiza vitanda hivyo kufungwa ndani ya masaa mawili na kuanza kutumiwa na wagonjwa waliokuwa.

Msikilize hapa waziri Ummy Mwalimu akitaja majina ya wakurugenzi waliosimamishwa:-

Waziri Ummy Mwalimu akisaidia kufagia