Ijumaa , 24th Jul , 2020

Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa kiume ya chama cha waandishi wa habari za soka FWA.

Henderson akibusu kombe la EPL

Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa kiume ya chama cha waandishi wa habari za soka FWA.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30, aliyeiongoza Liverpool kutwaa ubingwa wa kwanza wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza baada ya miaka 30 msimu huu, alipata zaidi ya robo za kura.

"Nina deni kubwa kwa watu wengi lakini hakuna zaidi ya wachezaji wenzangu wa sasa, ambao wamekuwa wazuri na wanastahili hii kila kidogo kama mimi." Alisema Henderson

Henderson pia kwa mara ya kwanza alitwaa kombe la klabu bingwa ya Dunia akiwa na Liverpool mwezi Desemba mwaka uliopita.

Wachezaji wenza wa Liverpool Virgil van Dijk na Sadio Mane, kiungo wa Manchester City Kevin de Bruyne na Mshambuliaji wa  Manchester United Marcus Rashford nao walimaliza kwenye tano bora.