Kaya 100 zakosa Makazi Uvinza baada ya mvua kubwa
Zaidi ya familia mia moja katika kijiji cha Kirando kata ya Sunuka wilayani Uvinza mkoani Kigoma hazina makazi baada ya nyumba zaidi ya 50 kuezuliwa na kubomoka kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa masaa sita usiku ambayo imeleta uharibifu wa mali.

