Serikali kuwakamata wanaowaficha wahamiaji haramu
Kutokana na tatizo la wahamiaji haramu kuendelea kuingia nchini na kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani, serikali imeanza kudhibiti vitendo hivyo kwa kuongeza ulinzi maeneo ya mipakani.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Mwigulu Nchemba wakati akizungumza na East Africa Radio kuhusu kuongezeka kwa wimbi la wahamiaji haramu nchini ambapo washiriki wakuu wanaowasaidia wahamiaji hao kuingia nchini ni baadhi ya watanzania ambao si waaminifu wanawaingiza wahamiaji hao na kuwahifandhi kwenye majumba yao kinyume cha sheria ya nchi inavyoelekeza.

.jpg?itok=50u-AUKv)