Kamanda Sirro; Ombeni picha za mnaowapangisha.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa pamoja na wenye nyumba za kupangisha jijini Dar es Salaam kuhakikisha kuwa wanakuwa na picha za wapangishaji wanaopangisha katika nyumba zao kwasababu za usalama.