Sakata la hujuma ya uchaguzi Yanga latua TAKUKURU.
Baada ya kukamata clip ya sauti ya baadhi ya wadau wa soka wakizungumza na kupanga mpango wa kuhujumu uchaguzi mkuu wa klabu ya soka ya Yanga hii leo ,Uongozi wa klabu hiyo umewasilisha rasmi malalamiko yao TAKUKURU ili ufanyike uchunguzi wa kina.