Wamorocco kuwachezesha wenyeji Mo Bejaia na Yanga
Marefa wa Morocco wameteuliwa kuchezesha mechi ya ufunguzi ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika kati ya wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia na Yanga SC ya Tanzania Juni 19 mwaka huu Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia,Algeria.