Wednesday , 29th Jun , 2016

Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu amesema kwamba wakuu wa wilaya walioteuliwa wengi ni vijana hivyo watu wasiwabeze kwa kuwa ukuu wa wilaya hauna umri bali kinachotakiwa ni wakuu hao kuuchapa kazi na kuleta maendeleo katika maeneo hayo.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akizungumza na wakuu wa wilaya ambao walioteuliwa na Rais wa Jam,huri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni

‘’Kazi hii hakuna mkubwa wala mdogo pia someni alama za nyakati, nyakati zimebadilika hivyo hakikisheni mnawahudumia wananchi vizuri’’ Amesema Mama Samia.

Wakuu wa wilaya mliobaki chapeni kazi yaliyopita si ndwele tugange yajayo hakikisheni mnafanya vizuri kiliko hapo mwanzo.

Aidha Makamu wa Rais amewaasa wakuu wa wilaya kwamba serikali haitaki kusikia kwamba mkuu wa wilaya anaomba chakula kwa ajili ya wananchi wake hivyo wafanye kazi na kuhakikisha wananchi wanaowaongoza wanafanya kazi.