Tutawalinda watoto wa Tanzania- Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema serikali itawalinda watoto dhidi ya matukio yanayowapata katika familia na yoyote atakayefanya ukatili dhidi ya mtoto sheria itachukua mkondo wake.