China kuisaidia Tanzania kwenye ujenzi wa viwanda
Serikali ya China imeichagua Tanzania kuwa nchi ya mfano katika utekelezaji wa mpango wake wa kuhamishia viwanda barani Afrika katika kipindi ambacho Tanzania nayo imekuwa ikihamasisha ujenzi wa viwanda kama msingi na mhimili mkuu wa uchumi.
