Watoto maskini milioni 69 hatarini kufariki
Kutokana na mwelekeo wa sasa, watoto milioni 69 watafariki dunia mpaka ifikapo 2030 kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika, huku watoto milioni 167, wakiishi katika umaskini, iwapo dunia haitaangazia zaidi hatma ya watoto maskini.