DC Kasesela kusaidia Lipuli FC kutinga Ligi Kuu
Katika kuhakikisha mkoa wa Iringa unapata klabu ya ligi kuu ya soka Tanzania bara mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka viongozi wa klabu hiyo kuweka pembeni tofauti zao na kuungana kwa pamoja ili kuepukana na aibu ya kila mwaka.
