Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela
Kasesela amesema amewaambia wadau wa mpira mkoa wa Iringa kwamba kumekua na changamoto kubwa kwa sasa kutokana na hali halisi ya kiuchumi hali inayopeleka viongozi klabuni hapo kurushiana mpira wa lawama kusaka mchawi wao .
''Ugomvi mnaouona sasa ni kwa kuwa tupo huku chini lakini tukishikamana tukahakikisha timu yetu inakwenda ligi kuu malumbano yatapungua na tutajikita kuhakikisha timu yetu inafanya vizuri''- Amesema Kasesela.
Aidha Kasesela amewataka wadau wa mpira waliomo mkoani Iringa na ambao wapo nje ya mkoa huo kushikamana kwa pamoja ili kuhakikisha timu yao inapanda daraja kwa kuichangia fedha na kutoa mali zao kwa hali na mali.


