Waandamana kupinga mauaji ya kiholela Kenya
Mamia ya watu wameandama jana katika mji mkuu Nairobi, Kenya kulaani mauaji ya kiholela kufuatia kuuawa kwa watu watatu wiki iliyopita akiwemo wakili wa kutetea haki za binadamu Willie Mwangi aliyekuwa mkosoaji wa ukiukaji unaofanywa na polisi.