Watu 33 kati 100 Tabora hawajakula
Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ameonesha wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la kiwango cha umaskini nchini, akiongea na wananchi wa Tabora amesema kuwa hali imezidi kuwa mbaya licha ya rasilimali lukuki zilizopo kwenye baadhi ya mikoa.