''Majeraha yalinipa kiu ya mafanikio'' - Chilunda
Mshambuliaji wa Azam FC Shaaban Idd Chilunda amesema majeraha aliyoyapata mwanzoni mwa msimu uliopita, ambayo yalimweka nje kwa raundi yote ya kwanza ya ligi kuu ndio chanzo cha yeye kufanya vizuri baada ya kupona.