Walioshtukiwa na Rais Magufuli waanza 'kukiona'
Watuhumiwa 12 wakiwemo wafanyabishara wanne na Askari polisi nane waliohusika na utoroshaji wa madini aina ya dhahabu kilo 319.59 yenye thamani ya kiasi cha shillingi bilioni 27 kinyume na sheria ya usafirishaji wa Madini nchini leo wamefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza.

