Watatu wafariki sababu ya Mvua, RC atoa neno
Mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Rukwa zimeendelea kusababisha maafa baada ya kusomba madaraja manne katika barabara ya Kasansa – Kilyamatundu inayounganisha mikoa ya Songwe, Rukwa na Katavi iliyopo bonde la ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga huku ikisababisha vifo vya watu watatu

