'Wasipotii agizo lazima wakamatwe' - DC Sabaya
Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, amewataka wamiliki wawili wa mabasi ya Machame Safari na Lim Safari, wahakikishe wanafika Kituo cha Polisi kama alivyowaagiza na kwamba yeye hajibizani na watu kwenye mitandao na wasipotii agizo lake watakamatwa kama wahalifu wengine.

