Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Wakulima waomba kuwahishiwa mbolea

Saturday , 10th Dec , 2022

Wakulima mkoani Geita wameiomba serikali kuwawaishia Mbolea kabla ya kilimo zitakazowawezesha kuendana na msimu wa kipindi husika ili waweze kufanya kilimo chenye tija kitakachobadilisha uchumi wao

Wakulima wameyasema hayo kwenye kongamano la miaka 61 ya uhuru mkoani Geita na kuiomba serikali iweze kuleta miradi ya umwagiliaji Maji ili waweze kufanya kilimo chenye kuleta maendeleo kwa jamii

"Kwa upande wa kilimo tunashukuru kinaendelea lakini sasa upande wa hali ya hewa, tabia ya nchi inachanganya na bei zinachanganya yani sisi wakulima wakati mwingine tunapata kikwazo kidogo kwa sababu ya utaratibu bei hazijawa Sawa sawa, hapo serikali ijitathimini vizuri kusudi wakulima tupate nafasi nzuri ya kupata mapato mazuri, kutuongezea Mbolea na kutuwaishia Mbolea kabla hatujaanza kilimo", alisema Nkingwa.

"Miaka 61 imepiga hatua kubwa sana kuna maendeleo mazuri na tunaomba viongozi wetu waweze kujikita kwenye maendeleo ili watanzania waweze kunufaika", alisema Thomas 

Afisa mipango halmashauri ya mji Geita Ndalo Samson anasema kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi zao kuu la biashara (Pamba), limeendelea kushuka huku akitoa ushauri wa mazao mbadala yatakayoendana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

"Hali ya uzalishaji wa zao hili umekuwa ukishuka mwaka hadi mwaka kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na bei ya soko  la dunia hata hivyo wananchi  wanahanasishwa kulima mazao mengine mbadala ya biashara  hasa zao la Alizeti", alisema Samson.

Mkuu wa wilaya ya Geita Wilson Shimo amewataka wananchi kuwa wamoja ili serikali inapoleta miradi ya maendeleo iweze kufanikiwa kwa urahisi.

"Tukibaguana tukatengana tukasema huyu ni mtaalam, tukasema huyu ni mwanasiasa tukasema huyu ni wakike huyu wakiume, tukasema huyu ni mkristo  huyu kuislam, huyu ni wa bara huyu ni wa visiwani na huyu wa CCM huyu wa Chadema tunakwenda kubaguana kusiko na sababu kwahiyo tusitengwe na vitu hivi ambavyo nimevitaja", alisema Shimo
 

HABARI ZAIDI

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Wanahabari wasisitizwa kuzingatia maadili ya kazi

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC atangaza msako kuwaondoa walinzi wazee kazini