Makazi ya binti aliyebakwa
Akisimulia kwa masikitiko tukio hilo la kubakwa kwa binti yake mama mzazi wa mtoto huyo anasema binti yake ana ulemavu huo unaomfanya muda wote kulala tuu kwani alipooza mwili akiwa na wiki tatu tangu alipozaliwa kwake.
Nae Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Butiama Devotha Paschal, amesema kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na kukithiri kwa vitendo vya ukatili wilayani humo huku mwanaasheria kutoka asasi isiyo ya kiserikali ya ATFGM Masanga Irene Assey, akikemea vikali juu ya vitendo hivyo vya ubakaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibubwa anasema alipata taarifa ya tukio hilo la ubakaji na kushirikiana na familia katika kukamata mhalifu.