Kushoto ni Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba na kulia ni Mbunge Luhaga Mpina
Swali la mbunge Luhaga Mpina lilitaka kujua sababu zilizopelekea kesi 1,097 za kodi za muda mrefu, zenye thamani ya Trilioni 360 na dola za Marekani milioni 181.4 kutoamuliwa hadi sasa, ambapo awali lilijibiwa na Naibu Waziri wa Fedha na halikumridhisha mbunge huyo na ndipo Spika wa Bunge akaingilia kati.
"Mhe. Spika, Trilioni 360 hazipo kwenye 'TRAB' na 'TRAT' ni kitu tofauti kabisa, hazipo kwenye mashauri ya kikodi ya, ya, ya, ya ya ya ya ya ya 'TRAB na TRAT' hili ni jambo mahususi lililokuwepo kwenye mzozo wa serikali na Barrick,", amejibu Waziri Nchemba.
Tazama video hapa chini