Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Uchimbaji madini maeneo ya hifadhi

Sunday , 3rd Jul , 2022

Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko amesema kuwa maeneo yaliyopo kwenye hifadhi bado yanatafutiwa ufumbuzi ili wachimbaji wa madini waweze kuchimba na kunufaika na rasilimali hizo.

Dkt. Biteko amesema hayo alipotembelea na kuzungumza na wachimbaji wadogo katika eneo la Lugelele wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya katika ziara yenye lengo ya kukagua shughuli za uchimbaji madini na kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji hao wa madini ya dhahabu.

Ameongeza kuwa, Serikali inayatafutia ufumbuzi maeneo yaliyopo kwenye hifadhi ili kuwawezesha wachimbaji na hivyo kunufaika na rasilimali madini.

Amefafanua kuwa, maeneo yaliyopo chini ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA) bado hayaruhisiwi kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo mpaka sasa. Aidha, kwenye hifadhi za misitu amefafanuwa kuwa, Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) haijazuia shughuli za uchimbaji madini.

"Maeneo ya hifadhi ya wanyamapori hakuruhusiwi shughuli za kibinadamu, za uchimbaji madini zinazoruhusiwa ni za aina mbili tu, kutafiti mafuta na gesi na kuchimba madini ya nishati," amesisitiza Dkt.Biteko.

Ameongeza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anataka kuwaona wachimbaji wanapewa fursa kwenye uchimbaji wa madini ili waweze kunufaika na rasilimali madini.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune amesema kuwa, shughuli za uchimbaji madini katika wilaya hiyo zimekuwa fursa kwa wananchi katika kujipatia kipato cha kila siku.

Amesema, wachimbaji wengi wanapata ajira katika maeneo hayo na amemweleza Waziri Biteko kuwa, wilaya ya Mbarali inapata wastani wa kilo 2.5 ya dhahabu ambayo huchangia kwenye Pato la Taifa na halmashauri hiyo.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko ametembelea kiwanda cha kuzalisha kokoto cha TAZARA Kongolo Quarry ili kujionea shughuli zinazofanyika katika kiwanda hicho.

HABARI ZAIDI

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Wanahabari wasisitizwa kuzingatia maadili ya kazi

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC atangaza msako kuwaondoa walinzi wazee kazini