Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Tetesi za usajili, Antony anauzwa Bilioni 200

Tuesday , 28th Jun , 2022

Taarifa za usajili barani Ulaya leo Juni 28, 2022. Miongoni mwa taarifa Chelsea inakaribia kumsajili Sterling kutoka Mnchester City, Ajax wataja dau la kumuuza Antony ni pauni milioni 70 na hatma ya Dembele ndani ya Barcelona kujulikana ndani ya masaa 72 yajayo.

Antony anauzwa Bilioni 200

Klabu ya Chelsea ipo kwenye mpango  wa kusajili wachezaji wawili kutoka Manchester City mshambuliaji Raheem Sterling na beki Nathan Ake. Kwa mujibu wa ripoti Chelsea imefanya mazungumzo na City juu ya nia yakutaka kuwasajili wachezaji hao na tayari Raheem Sterling ameongea na kocha wa Chelsea Thomas Tuchel na kampa mpango kazi namna anavyotaka kumtumia. Mkataba wa Sterling ndani ya Manchester City unamalizika mwakani 2023 na City wapo tayari kumuuza msimu huu ili asiondoke bure mwakani.

Ndani ya masaa 72 yajayo inatarajiwa winga wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Barcelona Ousmane Dembele atafanya maamuzi juu ya hatma yake kama anabaki Barcelona au anaondoka klabu hapo. Mkataba wa Dembele na Barcelona unamalizika mwishoni mwa mwezi huu June 30, 2022. Mkataba mpya ambao Barcelona wanataka kumpa mchezaji huyo haujaboreshwa kwenye kipengele cha mshahara na utabaki ule ule kama ilivyo kwenye mkataba wa sasa na yeye anataka ongezeko la mshahara. Vilabu vya Bayern Munich ya Ujerumani, Chelsea ya England  na PSG ya Ufaransa vyote vimeonyesha nia yakutaka kumsajili winga huyo.

Klabu ya Ajax ya Uholanzi ipo tayari kumuuza kiungo wake mshambuliaji raia wa Brazil Antonty kwa dau la Pauni miloni 70 kama ada ya uhamisho ambayo ni zaidi ya Bilioni 200 kwa pesa ya Tanzania (200,277,202,881.61). Manchester United ndio timu pekee iliyoonyesha nia yakutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. Manchester United bado hawajafanya usajili wa mchezaji hata mmoja mpaka sasa wakiwa chini ya kocha mpya Eric ten Hag na tayari kikosi hicho kimeanza maandalizi ya msimu mpya (Pre-season). Na kama wakifikia dau hilo basi wanaweza kumfanya mchezaji huyo kuwa usajili wa kwanza msimu huu.

Arsenal imepeleka offa ya pauni million 35 zaidi ya Bilioni 100 kwa pesa ya Tanzania kwa klabu ya Ajax kama ada ya uhamisho ya beki Lisandro Martinez raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 24. Arsenal wapo kwenye vita ya kumuwania mchezaji huyo na Manchester United ambao nao wanataka huduma ya beki huyo lakini Arsenal wananafasi kubwa ya kuinasa saini ya mchezaji huyu kuliko Manchester United. Kwa mujibu wa ripoti Ajax watamuuza  Martinez kwa ada ya Pauni milioni 45 zaidi ya Bilioni 124 kwa pesa ya Tanzania.

HABARI ZAIDI

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala