Thursday , 16th May , 2024

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetoa siku 90 kwa wamiliki wa hospitali, zahanati na vituo vya afya kuhakikisha wanaweka miundombinu madhubuti ya kuteketeza na kuhifadhi taka kwa mujibu wa sheria.

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 16, 2024 na Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC, na kusema kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya vifaa vya hospitali vilivyotumika kukutwa kwenye fukwe za bahari jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

"Tunatoa siku 90 kwa wote wenye zahanati, vituo vya afya na hospitali kuweza kuweka miundombinu madhubuti iliyopitishwa na Wizara ya Afya ya kuteketeza na kuhifadhi taka la sivyo wawape taka hizo wakandarasi waliosajiliwa na wana maeneo ya uteketezaji,"ameeleza Kaimu Mkurugenzi