
Msanii wa filamu Tausi Mdegela akiwa na mtoto wake wa kike
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Tausi Mdegela amesema, mwanaye anaendelea vizuri na muda wote yupo naye.
"Raha sana kuwa na kitu unachokitegemea halafu ukakipata, kwa sababu mtoto unaanza kuongea naye tangu yupo tumboni, ila mwanangu ananikataa sana ana-enjoy akiwa na baba yake, anaweza akawa ananyonya ila akishafika baba yake anaacha anakuwa na furaha kisha anacheka kwa nguvu" amesema Tausi
Aidha ameendelea kusema "Siwezi nikataja nataka watoto wangapi ila huyu akikua atapata mdogo wake na ndugu zake watafuata, pia siwezi nikasema nipate watoto wangapi maana itategemea uhai na mipango ya Mungu ila nitazaa mpaka pale itakaposhindikana".
Zaidi tazama akiongea kwenye video hapa chini.