Akizungumza jijini Dar es salaam, mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga, Jerry Muro amesema, katika mechi hiyo hawana mpango wa kuisaida timu yoyote katika michezo miwili iliyobakia.
Klabu hiyo inatarajia kukabidhiwa kombe lake katika mechi hiyo ambapo baada ya mchezo huo itaelekea mjini Mtwara kucheza mchezo wa mwisho wa ligi hiyo dhidi ya Ndanda FC itakayochezwa mkoani humo Mei tisa mwaka huu.