Kikosi cha mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Azam FC.
Mabingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara timu ya Azam fc ya jijini Dar es salaam imepata mwaliko toka baraza la vyama vya soka kwa nchini za afrika mashariki na kati CECAFA kwaajili ya kushiriki michuano ya klabu bingwa kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati maarufu kama kombe la Kagame michuano itakaayofanyika katikati ya mwezi ujao nchini Rwanda
Afisa habari wa timu hiyo Jafar Idd Maganga ‘mbunifu’ amesema ni kweli wamepokea mwaliko huo kutoka CECAFA wakiwaomba kushiriki michuano hiyo na wao kama timu wamepeleka ombi hilo kwa kocha mkuu naye atatoa mapendekezo yake kutokana na program zake katika timu hiyo na baadae uongozi wa timu hiyo utatangaza maamuzi ama mapendekezo ya kocha wao juu ya ushiriki katika michuano hiyo mikubwa kwa nagazi ya vilabu ukanda wa Afrika mashariki na kati.
Kwa upande mwingine Vilabu vya soka vya ligi kuu na daraja la kwanza ambavyo hivi sasa viko katika mchakato wa usajili kwaajili ya kuimarisha vikosi vyao vimetakiwa kufanya zoezi la usajili kwa kuzingatia mapendekezo ya makocha wa timu zao na pia kuwatumia makocha hao kukamilisha zoezi hilo
Afisa habari wa Azam fc Jafar Idd Maganga amesema kocha ndiye mtaalamu na anayejua mapungufu ya timu hivyo wanastahili kuachiwa jukumu hilo badala ya viongozi kufanya kazi hiyo kitu ambacho kitaalamu si sahii na ndio maana timu nyingi zinazotumia mtindo wa kila mtu kufanya usajili hujikuta zikifanya vibaya na baadae kupeleka lawama kwa makocha ambao hawakuwahusisha katika zoezi la usajili.