Tuesday , 10th Feb , 2015

Wakali wa muziki wa injili kutoka nchini Kenya, Daddy Owen pamoja na Papa Dennis wameendelea kuwajulisha mashabiki kazi yao ya upigaji picha za video yao ya Foundation ambayo wamekwenda kuifanyia huko London.

Daddy Owen pamoja na Papa Dennis wakiwa katika picha ya maandalizi

Mastaa hawa katika wakati wao huko London wameweza pia kufanya mambo mengine ikiwepo kukutana na staa mkubwa wa mpira kutoka Kenya, Victor Wanyama na pia kuweza kuhudhuria moja ya michezo ya timu anayochezea ya Southampton kama sehemu ya kuonesha kujivunia na kuwa pamoja na star huyo.

Video ya Foundation inatarajiwa kukamilika hivi karibuni na kuleta mapinduzi makubwa kabisa katika upande wa video za muziki Kenya kutokana na uwekezaji na mipango mikubwa ambayo wasanii hawa wamewekeza katika kazi hiyo.