Friday , 15th Apr , 2016

Gwiji la taarabu, Malkia Khadija Kopa yupo kwenye mchakato wa kuanzisha bendi kwa ajili ya familia yake.

Mwimbaji wa Taarabu, Khadija Kopa.

Akihojiwa na kipindi namba 1 cha burudani nchini (Enews) cha EATV ameeleza kuwa amechelewa kuanzisha bendi hiyo kwa sababu yeye ni mwajiriwa wa TOT na alikuwa na kazi nyingi sana.

Aidha alikuwa akifanya kazi kama bendi ingawa hakuwa na bendi, alikuwa anakodi wasanii anafanya nao kazi, anawalipa.

Amesisitiza kuwa watoto wake sasa wamekuwa waimbaji hivyo hana budi kutengeneza bendi kwa ajili yao.

Ameongeza kuwa anafanya hivyo kwa sababu itafika kipindi yeye ataacha muziki na kufanya shughuli nyingine tofauti na muziki.

Mwimbaji huyo wa miondoko ya taarabu amesema kuwa bendi hiyo itajumuisha pia wasanii wa nje ila ameitengeneza kifamilia kwasababu amewatengenezea watoto wake.