Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

TRA ruksa kutembea na polisi ukusanyaji kodi

Thursday , 20th Apr , 2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameibariki Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea kuwatumia TAKUKURU pamoja na Jeshi la Polisi wenye silaha za moto wakati wanapokwenda kukusanya mapato pamoja na kodi kwa wafanyabiashara ambao ni wanaodaiwa sugu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu Bungeni Mjini Dodoma, amesema ni sahihi kwa kikosi kazi hicho (task force) kutumika kwa kuwa wapo baadhi ya wafanyabiashara sugu wenye lengo baya la kutotaka kulipa madeni na badala yake hutoa rushwa.

Mhe. Lema alitaka kusikia kauli ya serikali juu ya mfumo unaotumiwa TRA wa kusumbua na kuwatisha wafanyabiashara katika shughuli zao za kila siku huku ikiwa inadaiwa kuwa mamlaka hiyo hutumia Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na TAKUKURU katika miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam, Mwanza , Arusha na Mbeya.

“Ni kweli kwamba tunacho chombo ambacho kinachowajibika katika ukusanyaji wa mapato na kodi kutoka kwa walipa kodi wetu wafanyabiashara wakiwemo, lakini TRA kutumia ‘task force’ haina maana ya kuwatishia amani wafanyabiashara ila lengo lake ni kufuatilia wadaiwa sugu japokuwa siyo wote ila wachache hawataki kabisa kulipa pamoja na kwamba wanajua wao ni wadaiwa sugu..... Tunatumia TAKUKURU kwa sababu kuna wengine hutumia fursa hiyo kutaka kuwahonga maafisa wa TRA ili wafutiwe madeni yao”. Alisema Majaliwa

Vile vile Majaliwa amesema ‘task force’ imeundwa na TRA wenyewe ili kuona wanapokwenda kukusanya madeni yao hakutumiki vitendo ambavyo havikubariki kama vile utoaji wa rushwa ili madeni hayo yasilipwe au namna nyingine yoyote ambayo mfanyabiashara anaweza kuona si sahihi kwake.

HABARI ZAIDI

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Wanahabari wasisitizwa kuzingatia maadili ya kazi

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC atangaza msako kuwaondoa walinzi wazee kazini