Tuesday , 27th Feb , 2018

Rais mpya wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza mabadiliko katika baraza lake la Mawaziri na kufanya mabadiliko makubwa. 

Rais Ramaphosa amemteuwa Nhlanhla Nene kuwa waziri wa fedha ambaye ahapo awali aliwahi kushika wadhifa huo katika utawala wa Jacob Zuma lakini baadae alifukuzwa.

Uteuzi wa  Nhlanhla Nene kurejea katika nafasi ya Waziri wa Fedha umepewa nafasi kubwa ukizingatia baada ya kufukuzwa mwezi Desemba mwaka 2015 na kusababisha hofu kwa wawekezaji  na kusababisha fedha ya nchi hiyo Rand kuporomoka.

Aidha rais huyo amemteua David Mabuzza, ambaye ni Naibu Rais wa chama tawala cha African National Congress (ANC) ameteuliwa kuwa naibu rais wa nchi hiyo, Nkosazana Dlamini-Zuma, mke wa zamani wa Jacob Zuma ameteuliwa kuwa waziri katika ofisi ya rais.

Baadhi ya Mawaziri waliokuwepo katika utawala uliopita wameendelea kushika nyadhifa hizo huku wengine wakiwa washirika wa karibu wa Rais Mstaafu Jacob Zuma wameachwa katika baraza hilo.

Ramaphosa, ambaye ni mfanyabiashara wa zamani  inadaiwa kuwa alitumia muda wake mwingi katika hotuba ya muelekeo wa taifa hilo kwa kutoa ahadi ya kupambana na rushwa, kuinua uchumi na kutengeneza ajira.