Tanzania ina ongezeko la ukatili kwa watoto
Jumla ya watoto 963 wamelawitiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita nchini Tanzania, huku sababu kuu ikitajwa kuwa ni ukatili unaofanywa dhidi yao pamoja na ukosefu wa mfumo bora na unaoeleweka wa kuwalinda watoto dhidi ya hatari na majanga.

