Hali ya majeruhi wa bomu Arusha inaimarika
Watu 17 waliojeruhiwa kwenye mapaja na miguuni na bomu lililorushwa kwenye baa ya Night Park mkoani Arusha jana wamelazwa katika hospitali ya mkoa Maunt Meru, huku mmoja akiwa amelazwa hospitali inayomilikiwa na kanisa la KKKT ya Selian.