Kaimu balozi wa Libya Dar ajiua kwa risasi
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania leo imepokea taarifa kutoka ubalozi wa Libya nchini ikieleza kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya Bw. Ismail Nwairat, amefariki dunia jana kwa kujipiga risasi.
Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya saa saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa Libya ambapo imeelezwa kuwa marehemu alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto.

