BMT yaitaka BFT kuandaa mapambano ya ndani
Baraza la michezo nchini BMT limeitaka Shirikisho la Ngumi nchini BFT kuweka kambi au kutafuta mapambano ya ndani kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya All African Games inayoanza kutimua vumbi Septemba mwaka huu nchini Congo Brazzaville.
