Kipindupindu chazidi kusambaa sasa ni Dar na Moro
Ugonjwa wa kipindupindu bado unaendelea kusambaa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, ambapo hadi kufikia leo kulikuwa na wagonjwa 38, ambao wamelazwa katika kambi maalumu za Mwananyamala na Mburahati.

