Sitaidharau TP Mazembe - Mbwana Samatta
Mara baada ya kukamilisha taratibu zote za kujiunga na klabu ya Genk,nyota Mbwana Samatta amesema alikuwa anahisi anakuwa chizi baada ya dili hilo kukamilika ambalo limeifanya ndoto yake ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya kukamilika.

