Watanzania watakiwa kuiombea Amani Zanzibar
Waumini wa dini nchini na Watanzania wametakiwa kuiombea Zanzibar ili iendelee kuwa na amani na utulivu kutokana na kukabiliwa na mvutano wa kisiasa baada ya Tume ya Uchaguzi visiwani humo kufuta matokeo ya Uchaguzi na kuamuru urudiwe.

