Utoaji mimba wachangia 16% ya vifo vya akina mama
Chama Cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA) kimesema idadi kubwa ya wanawake wanaokwenda katika vituo vya afya nchini mara baada ya mimba kuharibika ni wale waliotoa mimba katika njia zisizo salama na kuhatarisha maisha yao.

