Muongozo wa ukusanyaji ushahidi wazinduliwa.
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imewataka wataalam wa Maabara, Ustawi wa Jamii na Wahudumu wa Afya, waanze kutumia muongozo wa namna ya ukusanyaji wa sampuli kwa ajili ya ushahidi wa kimahakama kwa waliofanyiwa ukatili.