Wenger aanza kuibomoa Leicester city amtaka Vardy
Kocha Mkuu wa klabu ya Arsenal maarufu kama washika bunduki wa jiji la London Mfaransa Arsene Wenger ameanza kukimega kikosi cha mabingwa wa ligi kuu ya England EPL Leicester City akistukiza usajili wa mshambuliaji hatari wa timu hiyo Jamie Vardy.