Serikali kujenga viwanda vikubwa viwili vya mbolea
Naibu waziri wa wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi William Tate Ole-Nasha amesema serikali ipo katika mchakato wa kujenga viwanda viwili vikubwa vya mbolea nchini ili kukabiliana na tatizo la mbolea hapa nchini.