Bodi ya Utalii yasisitiza Mlima Kilimanjaro upo TZ
Mlima Kilimanjaro upo Mkoa wa Kilimanjaro Tanzania.
Bodi ya Utalii nchini imetoa taarifa kufafanua kuhusu mlima Kilimanjaro baada ya shirika moja la habari la Marekani kudaiwa kuchapisha taarifa iliyoonekana kuashiria mlima huo unapatikana Kenya.