Majaliwa ataka CDA itenge eneo la bandari kavu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa mkoa wa Dodoma pamoja na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kutenga eneo la bandari kavu ili mkoa huo uweze kupokea na kuhifadhi mizigo na kurahisisha biashara kwa mikoa jirani.

