Azam FC yabanwa mbavu Chamazi
Mabingwa wa soka kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati timu ya Azam FC, leo imeshindwa tena kuvuna point 3 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliopigwa katika dimba la Chamazi, Dar es Salaam, kwa kulazimishwa sare ya 2-2 na Ruvu Shooting.