Serikali yadhamiria kukuza Utalii na Kilimo
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amesema, Serikali imedhamiria kuimarisha sekta ya kilimo na Utalii ili ziweze kutoa mchango mkubwa kuinua uchumi wa Taifa pamoja na kuwaondoa wananchi wake kutoka katika lindi la umasikini.